Zaburi 132
Psalms 132 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Ee Bwana, mkumbuke Daudi
na taabu zote alizozistahimili. 2Aliapa kiapo kwa Bwana
na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo: 3“Sitaingia nyumbani mwangu
au kwenda kitandani mwangu: 4sitaruhusu usingizi katika macho yangu,
wala kope zangu kusinzia, 5mpaka nitakapompatia Bwana mahali,
makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” 6Tulisikia habari hii huko Efrathi,
tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara:* 7“Twendeni kwenye makao yake,
na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; 8inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia,
wewe na Sanduku la nguvu zako. 9Makuhani wako na wavikwe haki,
watakatifu wako na waimbe kwa furaha.” 10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako,
usimkatae mpakwa mafuta wako. 11Bwana alimwapia Daudi kiapo,
kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua:
“Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe
katika kiti chako cha enzi, 12kama wanao watashika Agano langu
na sheria ninazowafundisha,
ndipo wana wao watarithi
kiti chako cha enzi milele na milele.” 13Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni,
amepaonea shauku pawe maskani yake: 14“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele;
hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku: 15Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele:
nitashibisha maskini wake kwa chakula. 16Nitawavika makuhani wake wokovu,
nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha. 17“Hapa nitamchipushia Daudi pembe,*
na kuweka taa kwa ajili ya masiya* wangu. 18Adui zake nitawavika aibu,
bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.