Zaburi 133
Psalms 133 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza
wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! 2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,
yakitiririka kwenye ndevu,
yakitiririka kwenye ndevu za Aroni,
mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. 3Ni kama vile umande wa Hermoni
unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni.
Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake,
naam, hata uzima milele.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.