Zaburi 134
Psalms 134 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana,
ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana. 2Inueni mikono yenu katika pale patakatifu
na kumsifu Bwana. 3Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia,
awabariki kutoka Sayuni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.