Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Listen to Ezra 2
1Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa: 3wazao wa Paroshi 2,172 4wazao wa Shefatia 372 5wazao wa Ara 775 6wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812 7wazao wa Elamu 1,254 8wazao wa Zatu 945 9wazao wa Zakai 760 10wazao wa Bani 642 11wazao wa Bebai 623 12wazao wa Azgadi 1,222 13wazao wa Adonikamu 666 14wazao wa Bigwai 2,056 15wazao wa Adini 454 16wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98 17wazao wa Besai 323 18wazao wa Yora 112 19wazao wa Hashumu 223 20wazao wa Gibari 95 21watu wa Bethlehemu 123 22watu wa Netofa 56 23watu wa Anathothi 128 24watu wa Azmawethi 42 25wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743 26wazao wa Rama na Geba 621 27watu wa Mikmashi 122 28watu wa Betheli na Ai 223 29wazao wa Nebo 52 30wazao wa Magbishi 156 31wazao wa Elamu ile ingine 1,254 32wazao wa Harimu 320 33wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 725 34wazao wa Yeriko 345 35wazao wa Senaa 3,630 36Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973 37wazao wa Imeri 1,052 38wazao wa Pashuri 1,247 39wazao wa Harimu 1,017 40Walawi: wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 74 41Waimbaji: wazao wa Asafu 128 42Mabawabu wa lango la Hekalu: wazao wa //Shalumu, Ateri, Talmoni, //Akubu, Hatita na Shobai 139 43Watumishi wa Hekalu:* wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, 44wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni, 45wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu, 46wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani, 47wazao wa Gideli, Gahari, Reaya, 48wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu, 49wazao wa Uza, Pasea, Besai, 50wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu, 51wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri, 52wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha, 53wazao wa Barkosi, Sisera, Tema, 54wazao wa Nesia na Hatifa. 55Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda, 56wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli, 57wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami. 58Watumishi wa Hekalu wote na //wazao wa watumishi //wa Solomoni 392 59Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli: 60wazao wa //Delaya, Tobia na Nekoda 652 61Kutoka miongoni mwa makuhani: Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). 62Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.* 64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 65tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. 66Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, 67ngamia 435 na punda 6,720. 68Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 69Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000* za dhahabu, mane 5,000* za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo. 70Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.