Ezra 2:62
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
Ezra 2:62 in English
Ezra 2:62 · Berean Standard Bible
These men searched for their family records, but they could not find them and so were excluded from the priesthood as unclean.
Context
60wazao wa //Delaya, Tobia na Nekoda 652 61Kutoka miongoni mwa makuhani:
Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). 62Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.* 64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.