Native Bible

Psalms 120 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Listen to Zaburi 120
1Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu. 2Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu. 3Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu? 4Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu. 5Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari! 6Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani. 7Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.