Zaburi 121
Psalms 121 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Nayainua macho yangu nitazame vilima,
msaada wangu utatoka wapi? 2Msaada wangu hutoka kwa Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia. 3Hatauacha mguu wako uteleze,
yeye akulindaye hatasinzia, 4hakika, yeye alindaye Israeli
hatasinzia wala hatalala usingizi. 5Bwana anakulinda,
Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume, 6jua halitakudhuru mchana,
wala mwezi wakati wa usiku. 7Bwana atakukinga na madhara yote,
atayalinda maisha yako, 8Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka,
tangu sasa na hata milele.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.