Zaburi 122
Psalms 122 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,
“Twende nyumbani ya Bwana.” 2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama
malangoni mwako. 3Yerusalemu imejengwa vyema kama mji
ambao umeshikamanishwa pamoja. 4Huko ndiko makabila hukwea,
makabila ya Bwana,
kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo
waliopewa Israeli. 5Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa,
viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. 6Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:
“Wote wakupendao na wawe salama. 7Amani na iwepo ndani ya kuta zako
na usalama ndani ya ngome zako.” 8Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki,
nitasema, “Amani iwe ndani yako.” 9Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu,
nitatafuta mafanikio yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.