Zaburi 129
Psalms 129 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Wamenionea mno tangu ujana wangu;
Israeli na aseme sasa: 2wamenionea mno tangu ujana wangu,
lakini bado hawajanishinda. 3Wakulima wamelima mgongo wangu,
na kufanya mifereji yao mirefu. 4Lakini Bwana ni mwenye haki;
amenifungua toka kamba za waovu. 5Wale wote waichukiao Sayuni
na warudishwe nyuma kwa aibu. 6Wawe kama majani juu ya paa,
ambayo hunyauka kabla hayajakua; 7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,
wala akusanyaye kujaza mikono yake. 8Wale wapitao karibu na wasiseme,
“Baraka ya Bwana iwe juu yako;
tunakubariki katika jina la Bwana.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.