Zaburi 113
Psalms 113 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Msifuni Bwana.
Enyi watumishi wa Bwana msifuni,
lisifuni jina la Bwana. 2Jina la Bwana na lisifiwe,
sasa na hata milele. 3Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,
jina la Bwana linapaswa kusifiwa. 4Bwana ametukuka juu ya mataifa yote,
utukufu wake juu ya mbingu. 5Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu,
Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi, 6ambaye huinama atazame chini
aone mbingu na nchi? 7Huwainua maskini kutoka mavumbini,
na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala, 8huwaketisha pamoja na wakuu,
pamoja na wakuu wa watu wake. 9Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,
akiwa mama watoto mwenye furaha.
Msifuni Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.