Native Bible

Ezekiel 30:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kushi* na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya* na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

Ezekiel 30:5 in English

Ezekiel 30:5 · Berean Standard Bible

Cush, Put, and Lud,* and all the various peoples, as well as Libya and the men of the covenant land, will fall with Egypt by the sword.

Context

3Kwa kuwa siku ile imekaribia, siku ya Bwana imekaribia, siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa. 4Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa. 5Kushi* na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya* na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri. 6“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. Kutoka Migdoli hadi Aswani, watauawa ndani yake kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi. 7“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yao itakuwa magofu miongoni mwa miji iliyo magofu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.