Ezekieli 30:3
Ezekiel 30:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa siku ile imekaribia, siku ya Bwana imekaribia, siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.
Ezekiel 30:3 in English
Ezekiel 30:3 · Berean Standard Bible
For the day is near, the Day of the LORD is near. It will be a day of clouds, a time of doom for the nations.*
Context
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,
“Ole wa siku ile!” 3Kwa kuwa siku ile imekaribia,
siku ya Bwana imekaribia,
siku ya mawingu,
siku ya maangamizi kwa mataifa. 4Upanga utakuja dhidi ya Misri,
nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.
Mauaji yatakapoangukia Misri,
utajiri wake utachukuliwa
na misingi yake itabomolewa. 5Kushi* na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya* na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.