Native Bible

Ezekiel 30:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa.

Ezekiel 30:4 in English

Ezekiel 30:4 · Berean Standard Bible

A sword will come against Egypt, and there will be anguish in Cush * when the slain fall in Egypt, its wealth is taken away, and its foundations are torn down.

Context

2“Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ombolezeni ninyi na mseme, “Ole wa siku ile!” 3Kwa kuwa siku ile imekaribia, siku ya Bwana imekaribia, siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa. 4Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa. 5Kushi* na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya* na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri. 6“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. Kutoka Migdoli hadi Aswani, watauawa ndani yake kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.