Ezekieli 30:6
Ezekiel 30:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. Kutoka Migdoli hadi Aswani, watauawa ndani yake kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi.
Ezekiel 30:6 in English
Ezekiel 30:6 · Berean Standard Bible
For this is what the LORD says: The allies of Egypt will fall, and her proud strength will collapse. From Migdol to Syene * they will fall by the sword within her, declares the Lord GOD.
Context
4Upanga utakuja dhidi ya Misri,
nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.
Mauaji yatakapoangukia Misri,
utajiri wake utachukuliwa
na misingi yake itabomolewa. 5Kushi* na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya* na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri. 6“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo:
“ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka
na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.
Kutoka Migdoli hadi Aswani,
watauawa ndani yake kwa upanga,
asema Bwana Mwenyezi. 7“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa
miongoni mwa nchi zilizo ukiwa,
nayo miji yao itakuwa magofu
miongoni mwa miji iliyo magofu. 8Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimi Bwana,
nitakapoiwasha Misri moto
na wote wamsaidiao watapondwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.