Ezekieli 30:7
Ezekiel 30:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yao itakuwa magofu miongoni mwa miji iliyo magofu.
Ezekiel 30:7 in English
Ezekiel 30:7 · Berean Standard Bible
They will be desolate among desolate lands, and their cities will lie among ruined cities.
Context
5Kushi* na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya* na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri. 6“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo:
“ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka
na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.
Kutoka Migdoli hadi Aswani,
watauawa ndani yake kwa upanga,
asema Bwana Mwenyezi. 7“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa
miongoni mwa nchi zilizo ukiwa,
nayo miji yao itakuwa magofu
miongoni mwa miji iliyo magofu. 8Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimi Bwana,
nitakapoiwasha Misri moto
na wote wamsaidiao watapondwa. 9“ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.