Native Bible

Ezekiel 30:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,* ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali makundi ya wajeuri wa Thebesi.

Ezekiel 30:15 in English

Ezekiel 30:15 · Berean Standard Bible

I will pour out My wrath on Pelusium,* the stronghold of Egypt, and cut off the crowds of Thebes.

Context

13“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi* Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima. 14Nitaifanya Pathrosi* kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi* 15Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,* ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali makundi ya wajeuri wa Thebesi. 16Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima. 17Wanaume vijana wa Oni* na wa Pi-Besethi* wataanguka kwa upanga nayo hiyo miji itatekwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.