Ezekieli 30:17
Ezekiel 30:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wanaume vijana wa Oni* na wa Pi-Besethi* wataanguka kwa upanga nayo hiyo miji itatekwa.
Ezekiel 30:17 in English
Ezekiel 30:17 · Berean Standard Bible
The young men of On and Pi-beseth * will fall by the sword, and those cities will go into captivity.
Context
15Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,*
ngome ya Misri,
nami nitakatilia mbali
makundi ya wajeuri wa Thebesi. 16Nitaitia moto nchi ya Misri;
Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu.
Thebesi itachukuliwa na tufani,
Memfisi itakuwa katika taabu daima. 17Wanaume vijana wa Oni* na wa Pi-Besethi*
wataanguka kwa upanga
nayo hiyo miji itatekwa. 18Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza
nitakapovunja kongwa la Misri;
hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.
Atafunikwa na mawingu
na vijiji vyake vitatekwa. 19Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,
nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.