Ezekieli 30:19
Ezekiel 30:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu, nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”
Ezekiel 30:19 in English
Ezekiel 30:19 · Berean Standard Bible
So I will execute judgment on Egypt, and they will know that I am the LORD.”
Context
17Wanaume vijana wa Oni* na wa Pi-Besethi*
wataanguka kwa upanga
nayo hiyo miji itatekwa. 18Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza
nitakapovunja kongwa la Misri;
hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.
Atafunikwa na mawingu
na vijiji vyake vitatekwa. 19Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,
nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ” 20Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno la Bwana likanijia kusema: 21“Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.