Native Bible

Ezekiel 30:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima.

Ezekiel 30:16 in English

Ezekiel 30:16 · Berean Standard Bible

I will set fire to Egypt, Pelusium will writhe in anguish, Thebes will be split open, and Memphis will face daily distress.

Context

14Nitaifanya Pathrosi* kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi* 15Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,* ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali makundi ya wajeuri wa Thebesi. 16Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima. 17Wanaume vijana wa Oni* na wa Pi-Besethi* wataanguka kwa upanga nayo hiyo miji itatekwa. 18Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza nitakapovunja kongwa la Misri; hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma. Atafunikwa na mawingu na vijiji vyake vitatekwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.