Native Bible

Ezekiel 30:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitaifanya Pathrosi* kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi*

Ezekiel 30:14 in English

Ezekiel 30:14 · Berean Standard Bible

I will lay waste Pathros, set fire to Zoan, and execute judgment on Thebes.*

Context

12Nitakausha vijito vya Naili na nitaiuza nchi kwa watu waovu, kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilichomo ndani yake. Mimi Bwana nimenena haya. 13“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi* Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima. 14Nitaifanya Pathrosi* kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi* 15Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,* ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali makundi ya wajeuri wa Thebesi. 16Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.