Ezekieli 30:12
Ezekiel 30:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitakausha vijito vya Naili na nitaiuza nchi kwa watu waovu, kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilichomo ndani yake. Mimi Bwana nimenena haya.
Ezekiel 30:12 in English
Ezekiel 30:12 · Berean Standard Bible
I will make the streams dry up and sell the land to the wicked. By the hands of foreigners I will bring desolation upon the land and everything in it. I, the LORD, have spoken.
Context
10“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri
kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. 11Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,
litaletwa ili kuangamiza nchi.
Watafuta panga zao dhidi ya Misri
na kuijaza nchi kwa waliouawa. 12Nitakausha vijito vya Naili
na nitaiuza nchi kwa watu waovu,
kwa mkono wa wageni,
nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu
kilichomo ndani yake.
Mimi Bwana nimenena haya. 13“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Nitaangamiza sanamu
na kukomesha vinyago katika Memfisi*
Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,
nami nitaeneza hofu katika nchi nzima. 14Nitaifanya Pathrosi* kuwa ukiwa
na kuitia moto Soani,
nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.