Native Bible

Ezekiel 30:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi* Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

Ezekiel 30:13 in English

Ezekiel 30:13 · Berean Standard Bible

This is what the Lord GOD says: I will destroy the idols and put an end to the images in Memphis.* There will no longer be a prince in Egypt, and I will instill fear in that land.

Context

11Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote, litaletwa ili kuangamiza nchi. Watafuta panga zao dhidi ya Misri na kuijaza nchi kwa waliouawa. 12Nitakausha vijito vya Naili na nitaiuza nchi kwa watu waovu, kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilichomo ndani yake. Mimi Bwana nimenena haya. 13“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi* Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima. 14Nitaifanya Pathrosi* kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi* 15Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,* ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali makundi ya wajeuri wa Thebesi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.