Ezekieli 30:11
Ezekiel 30:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote, litaletwa ili kuangamiza nchi. Watafuta panga zao dhidi ya Misri na kuijaza nchi kwa waliouawa.
Ezekiel 30:11 in English
Ezekiel 30:11 · Berean Standard Bible
He and his people with him, the most ruthless of the nations, will be brought in to destroy the land. They will draw their swords against Egypt and fill the land with the slain.
Context
9“ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja. 10“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri
kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. 11Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,
litaletwa ili kuangamiza nchi.
Watafuta panga zao dhidi ya Misri
na kuijaza nchi kwa waliouawa. 12Nitakausha vijito vya Naili
na nitaiuza nchi kwa watu waovu,
kwa mkono wa wageni,
nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu
kilichomo ndani yake.
Mimi Bwana nimenena haya. 13“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Nitaangamiza sanamu
na kukomesha vinyago katika Memfisi*
Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,
nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.