Native Bible

1 Kings 9:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi Hiramu alikuwa amempelekea mfalme talanta 120* za dhahabu.

1 Kings 9:14 in English

1 Kings 9:14 · Berean Standard Bible

And Hiram had sent the king 120 talents of gold.*

Context

12Lakini Hiramu alipotoka Tiro kwenda kuiona ile miji ambayo Solomoni alikuwa amempa, hakupendezwa nayo. 13Hiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?” Naye akaiita nchi ya Kabul,* jina lililoko hadi leo. 14Basi Hiramu alikuwa amempelekea mfalme talanta 120* za dhahabu. 15Haya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Solomoni, alivyowafanyiza watu ili kulijenga hekalu la Bwana, na jumba lake la kifalme, na Milo,* ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri. 16(Farao mfalme wa Misri alikuwa ameushambulia na kuuteka mji wa Gezeri. Alikuwa ameuchoma moto. Akawaua Wakanaani waliokuwa wakikaa humo na kisha kuutoa kwa binti yake, yaani mkewe Solomoni, kama zawadi ya arusi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.