Native Bible

Song of Songs 8:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani akimwegemea mpenzi wake?

Song of Songs 8:5 in English

Song of Songs 8:5 · Berean Standard Bible

Who is this coming up from the wilderness, leaning on her beloved?

Context

3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kuume unanikumbatia. 4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza: msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe. 5Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani akimwegemea mpenzi wake? 6(5) Nilikuamsha chini ya mtofaa, huko mama yako alipotunga mimba yako, huko yeye alipata utungu akakuzaa. (6) Nitie kama muhuri moyoni mwako, kama muhuri kwenye mkono wako; kwa maana upendo una nguvu kama mauti, wivu wake ni mkatili kama kuzimu. Unachoma kama mwali wa moto, kama mwali mkubwa wa moto wa Bwana hasa. 7Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, mito haiwezi kuugharikisha. Kama mtu angelitoa mali yote ya nyumbani mwake kwa ajili ya upendo, angelidharauliwa kabisa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.