Wimbo 8:4
Song of Songs 8:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Binti za Yerusalemu, ninawaagiza: msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.
Song of Songs 8:4 in English
Song of Songs 8:4 · Berean Standard Bible
O daughters of Jerusalem, I adjure you: Do not arouse or awaken love until the time is right.
Context
2Ningelikuongoza na kukuleta
katika nyumba ya mama yangu,
yeye ambaye amenifundisha.
Ningelikupa divai iliyokolezwa unywe,
asali ya maua ya mikomamanga yangu. 3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,
na mkono wake wa kuume unanikumbatia. 4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza:
msichochee wala kuamsha mapenzi
hata yatakapotaka yenyewe. 5Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani
akimwegemea mpenzi wake? 6(5) Nilikuamsha chini ya mtofaa,
huko mama yako alipotunga mimba yako,
huko yeye alipata utungu akakuzaa.
(6) Nitie kama muhuri moyoni mwako,
kama muhuri kwenye mkono wako;
kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
wivu wake ni mkatili kama kuzimu.
Unachoma kama mwali wa moto,
kama mwali mkubwa wa moto wa Bwana hasa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.