Native Bible

Song of Songs 1:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

(4) Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! (5) Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Solomoni. (6) Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.

Song of Songs 1:6 in English

Song of Songs 1:6 · Berean Standard Bible

(4) It is only right that they adore you. (5) I am dark, yet lovely, O daughters of Jerusalem, like the tents of Kedar, like the curtains of Solomon. (6) Do not stare because I am dark, for the sun has gazed upon me. My mother’s sons were angry with me; they made me a keeper of the vineyards, but my own vineyard I have neglected.

Context

4Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. 5(4) Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. 6(4) Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! (5) Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Solomoni. (6) Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha. 7Niambie, wewe ambaye ninakupenda, unalisha wapi kundi lako la kondoo na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela karibu na makundi ya rafiki zako? 8Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote, fuata nyayo za kondoo, na kulisha wana-mbuzi wako karibu na hema za wachungaji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.