Native Bible

Song of Songs 1:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

(4) Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai.

Song of Songs 1:5 in English

Song of Songs 1:5 · Berean Standard Bible

(4) We will rejoice and delight in you; we will praise your love more than wine.

Context

3Manukato yako yananukia vizuri, jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. Ndiyo sababu wanawali wanakupenda! 4Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. 5(4) Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. 6(4) Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! (5) Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Solomoni. (6) Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha. 7Niambie, wewe ambaye ninakupenda, unalisha wapi kundi lako la kondoo na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela karibu na makundi ya rafiki zako?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.