Native Bible

Song of Songs 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Niambie, wewe ambaye ninakupenda, unalisha wapi kundi lako la kondoo na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela karibu na makundi ya rafiki zako?

Song of Songs 1:7 in English

Song of Songs 1:7 · Berean Standard Bible

Tell me, O one I love, where do you pasture your sheep? Where do you rest them at midday? Why should I be like a veiled woman beside the flocks of your companions?

Context

5(4) Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. 6(4) Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! (5) Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Solomoni. (6) Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha. 7Niambie, wewe ambaye ninakupenda, unalisha wapi kundi lako la kondoo na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela karibu na makundi ya rafiki zako? 8Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote, fuata nyayo za kondoo, na kulisha wana-mbuzi wako karibu na hema za wachungaji. 9Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.