Wimbo 1:9
Song of Songs 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.
Song of Songs 1:9 in English
Song of Songs 1:9 · Berean Standard Bible
I compare you, my darling, to a mare among Pharaoh’s chariots.
Context
7Niambie, wewe ambaye ninakupenda,
unalisha wapi kundi lako la kondoo
na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri.
Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela
karibu na makundi ya rafiki zako? 8Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote,
fuata nyayo za kondoo,
na kulisha wana-mbuzi wako
karibu na hema za wachungaji. 9Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike
aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao. 10Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli,
shingo yako ikiwa na mikufu ya vito. 11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu,
vyenye kupambwa kwa fedha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.