Zaburi 8
Psalms 8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Ee Bwana, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Umeuweka utukufu wako
juu ya mbingu. 2Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao
umeamuru sifa,
kwa sababu ya watesi wako,
kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi. 3Nikiziangalia mbingu zako,
kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota,
ulizoziratibisha, 4mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria,
binadamu ni nani hata unamjali? 5Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni,
ukamvika taji ya utukufu na heshima. 6Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako;
umeweka vitu vyote chini ya miguu yake. 7Mifugo na makundi yote pia,
naam, na wanyama wa kondeni, 8ndege wa angani na samaki wa baharini,
naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari. 9Ee Bwana, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.