Native Bible

Psalms 69:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, wa kunituliza, lakini sikumpata.

Psalms 69:20 in English

Psalms 69:20 · Berean Standard Bible

Insults have broken my heart, and I am in despair. I looked for sympathy, but there was none, for comforters, but I found no one.

Context

18Njoo karibu uniokoe, nikomboe kwa sababu ya adui zangu. 19Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua. 20Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, wa kunituliza, lakini sikumpata. 21Waliweka nyongo katika chakula changu na walinipa siki nilipokuwa na kiu. 22Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, nayo iwe upatilizo na tanzi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.