Zaburi 40:6
Psalms 40:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu;* sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji.
Psalms 40:6 in English
Psalms 40:6 · Berean Standard Bible
Sacrifice and offering You did not desire, but my ears You have opened.* Burnt offerings and sin offerings You did not require.
Context
4Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,
asiyewategemea wenye kiburi,
wale wenye kugeukia miungu ya uongo. 5Ee Bwana Mungu wangu,
umefanya mambo mengi ya ajabu.
Mambo uliyopanga kwa ajili yetu
hakuna awezaye kukuhesabia;
kama ningesema na kuyaelezea,
yangekuwa mengi mno kuyaelezea. 6Dhabihu na sadaka hukuvitaka,
lakini umefungua masikio yangu;*
sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi
hukuzihitaji. 7Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja:
imeandikwa kunihusu katika kitabu. 8Ee Mungu wangu,
natamani kuyafanya mapenzi yako;
sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.