Native Bible

Psalms 40:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”

Psalms 40:8 in English

Psalms 40:8 · Berean Standard Bible

I delight to do Your will, O my God;* Your law is within my heart.”

Context

6Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu;* sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji. 7Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kunihusu katika kitabu. 8Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.” 9Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee Bwana, kama ujuavyo. 10Sikuficha haki yako moyoni mwangu; ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha upendo wako na kweli yako mbele ya kusanyiko kubwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.