Zaburi 40:4
Psalms 40:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.
Psalms 40:4 in English
Psalms 40:4 · Berean Standard Bible
Blessed is the man who has made the LORD his trust, who has not turned to the proud, nor to those who lapse into falsehood.*
Context
2Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,
kutoka matope na utelezi;
akaiweka miguu yangu juu ya mwamba
na kunipa mahali imara pa kusimama. 3Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,
wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa
na kuweka tumaini lao kwa Bwana. 4Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,
asiyewategemea wenye kiburi,
wale wenye kugeukia miungu ya uongo. 5Ee Bwana Mungu wangu,
umefanya mambo mengi ya ajabu.
Mambo uliyopanga kwa ajili yetu
hakuna awezaye kukuhesabia;
kama ningesema na kuyaelezea,
yangekuwa mengi mno kuyaelezea. 6Dhabihu na sadaka hukuvitaka,
lakini umefungua masikio yangu;*
sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi
hukuzihitaji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.