Native Bible

Psalms 16:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.

Psalms 16:3 in English

Psalms 16:3 · Berean Standard Bible

As for the saints in the land, they are the excellence in whom all my delight resides.

Context

1Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia. 2Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.” 3Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. 4Huzuni itaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu. 5Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.