Native Bible

Psalms 125 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Listen to Zaburi 125
1Wale wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele. 2Kama milima inavyozunguka Yerusalemu, ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake sasa na hata milele. 3Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi waliopewa wenye haki, ili wenye haki wasije wakatumia mikono yao kutenda ubaya. 4Ee Bwana, watendee mema walio wema, wale walio wanyofu wa moyo. 5Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka, Bwana atawafukuza pamoja na watenda mabaya. Amani iwe juu ya Israeli.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.