Zaburi 124
Psalms 124 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Kama Bwana asingalikuwa upande wetu;
Israeli na aseme sasa: 2kama Bwana asingalikuwa upande wetu,
wakati watu walipotushambulia, 3wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu,
wangalitumeza tungali hai, 4mafuriko yangalitugharikisha,
maji mengi yangalitufunika, 5maji yaendayo kasi
yangalituchukua. 6Bwana asifiwe,
yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao. 7Tumeponyoka kama ndege
kutoka mtego wa mwindaji;
mtego umevunjika,
nasi tukaokoka. 8Msaada wetu ni katika jina la Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.