Native Bible

Psalms 119:81 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.

Psalms 119:81 in English

Psalms 119:81 · Berean Standard Bible

My soul faints for Your salvation; I wait for Your word.

Context

79Wale wakuchao na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako. 80Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe. 81Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako. 82Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?” 83Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.