Native Bible

Psalms 104:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu.

Psalms 104:15 in English

Psalms 104:15 · Berean Standard Bible

wine that gladdens the heart of man, oil that makes his face to shine, and bread that sustains his heart.

Context

13Huinyeshea milima kutoka orofa zake, dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake. 14Huyafanya majani ya mifugo yaote, na mimea kwa watu kulima, wajipatie chakula kutoka ardhini: 15divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu. 16Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. 17Humo ndege hufanya viota vyao, korongo ana nyumba yake kwenye msunobari.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.