Native Bible

Psalms 104:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.

Psalms 104:16 in English

Psalms 104:16 · Berean Standard Bible

The trees of the LORD have their fill, the cedars of Lebanon that He planted,

Context

14Huyafanya majani ya mifugo yaote, na mimea kwa watu kulima, wajipatie chakula kutoka ardhini: 15divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu. 16Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. 17Humo ndege hufanya viota vyao, korongo ana nyumba yake kwenye msunobari. 18Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu, majabali ni kimbilio la pelele.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.