Mithali 29:7
Proverbs 29:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo.
Proverbs 29:7 in English
Proverbs 29:7 · Berean Standard Bible
The righteous consider the cause of the poor, but the wicked have no regard for such concerns.
Context
5Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili,
anautandaza wavu kuitega miguu yake. 6Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe
bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi. 7Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini,
bali mwovu hajishughulishi na hilo. 8Wenye mzaha huuchochea mji,
bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira. 9Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu,
mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.