Native Bible

Proverbs 29:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi.

Proverbs 29:6 in English

Proverbs 29:6 · Berean Standard Bible

An evil man is caught by his own sin, but a righteous one sings and rejoices.

Context

4Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza. 5Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake. 6Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi. 7Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo. 8Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.