Mithali 17:21
Proverbs 17:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni; hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.
Proverbs 17:21 in English
Proverbs 17:21 · Berean Standard Bible
A man fathers a fool to his own grief; the father of a fool has no joy.
Context
19Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi;
naye ainuaye sana lango lake* hutafuta uharibifu. 20Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa;
naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu. 21Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni;
hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu. 22Moyo wenye furaha ni dawa nzuri,
bali roho iliyopondeka hukausha mifupa. 23Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri
ili kupotosha njia ya haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.