Native Bible

Job 41:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini.

Job 41:9 in English

Job 41:9 · Berean Standard Bible

Surely hope of overcoming him is false. Is not the sight of him overwhelming?

Context

7Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki? 8Kama ukiweka mkono wako juu yake, utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena! 9Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini. 10Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza. Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu? 11Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.