Yeremia 6:4
Jeremiah 6:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Jiandaeni kwa vita dhidi yake! Inukeni tumshambulie mchana! Lakini, ole wetu, mchana unaisha, na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu.
Jeremiah 6:4 in English
Jeremiah 6:4 · Berean Standard Bible
‘Prepare for battle against her; rise up, let us attack at noon. Woe to us, for the daylight is fading; the evening shadows grow long.
Context
2Nitamwangamiza Binti Sayuni,
aliye mzuri sana na mwororo. 3Wachungaji pamoja na makundi yao
watakuja dhidi yake;
watapiga mahema yao kumzunguka,
kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” 4“Jiandaeni kwa vita dhidi yake!
Inukeni tumshambulie mchana!
Lakini, ole wetu, mchana unaisha,
na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu. 5Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku,
na kuharibu ngome zake!” 6Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:
“Kateni miti mjenge boma
kuzunguka Yerusalemu.
Mji huu ni lazima uadhibiwe,
umejazwa na uonevu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.