Yeremia 6:2
Jeremiah 6:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitamwangamiza Binti Sayuni, aliye mzuri sana na mwororo.
Jeremiah 6:2 in English
Jeremiah 6:2 · Berean Standard Bible
Though she is beautiful and delicate, I will destroy the Daughter of Zion.*
Context
1“Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini!
Kimbieni kutoka Yerusalemu!
Pigeni tarumbeta katika Tekoa!
Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu!
Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini,
na uharibifu wa kutisha. 2Nitamwangamiza Binti Sayuni,
aliye mzuri sana na mwororo. 3Wachungaji pamoja na makundi yao
watakuja dhidi yake;
watapiga mahema yao kumzunguka,
kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” 4“Jiandaeni kwa vita dhidi yake!
Inukeni tumshambulie mchana!
Lakini, ole wetu, mchana unaisha,
na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.