Native Bible

Jeremiah 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wachungaji pamoja na makundi yao watakuja dhidi yake; watapiga mahema yao kumzunguka, kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.”

Jeremiah 6:3 in English

Jeremiah 6:3 · Berean Standard Bible

Shepherds and their flocks will come against her; they will pitch their tents all around her, each tending his own portion:

Context

1“Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini! Kimbieni kutoka Yerusalemu! Pigeni tarumbeta katika Tekoa! Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu! Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini, na uharibifu wa kutisha. 2Nitamwangamiza Binti Sayuni, aliye mzuri sana na mwororo. 3Wachungaji pamoja na makundi yao watakuja dhidi yake; watapiga mahema yao kumzunguka, kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” 4“Jiandaeni kwa vita dhidi yake! Inukeni tumshambulie mchana! Lakini, ole wetu, mchana unaisha, na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu. 5Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku, na kuharibu ngome zake!”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.