Native Bible

Jeremiah 6:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku, na kuharibu ngome zake!”

Jeremiah 6:5 in English

Jeremiah 6:5 · Berean Standard Bible

Rise up, let us attack by night and destroy her fortresses!’”

Context

3Wachungaji pamoja na makundi yao watakuja dhidi yake; watapiga mahema yao kumzunguka, kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” 4“Jiandaeni kwa vita dhidi yake! Inukeni tumshambulie mchana! Lakini, ole wetu, mchana unaisha, na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu. 5Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku, na kuharibu ngome zake!” 6Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Kateni miti mjenge boma kuzunguka Yerusalemu. Mji huu ni lazima uadhibiwe, umejazwa na uonevu. 7Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, ndivyo anavyomwaga uovu wake. Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake, ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.