Native Bible

Jeremiah 6:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, ndivyo anavyomwaga uovu wake. Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake, ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.

Jeremiah 6:7 in English

Jeremiah 6:7 · Berean Standard Bible

As a well gushes its water, so she pours out her evil. Violence and destruction resound in her; sickness and wounds are ever before Me.

Context

5Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku, na kuharibu ngome zake!” 6Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Kateni miti mjenge boma kuzunguka Yerusalemu. Mji huu ni lazima uadhibiwe, umejazwa na uonevu. 7Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, ndivyo anavyomwaga uovu wake. Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake, ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima. 8Pokea onyo, ee Yerusalemu, la sivyo nitageukia mbali nawe na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa, asiweze mtu kuishi ndani yake.” 9Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli kwa uangalifu kama kwenye mzabibu; pitisha mkono wako kwenye matawi tena, kama yeye avunaye zabibu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.